Mafuriko Jangwani, Hali ni Mbaya, Makonda Atinga Kushuhudia – VIDEO

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam, zimesababisha maafa makubwa ikiwemo mafuriko katika eneo la Jangwani, ambapo hali imeonekana kuwa mbaya zaidi kiasi cha watu kushindwa kuvuka upande mmoja kwenda mwingine huku baadhi ya nyumba zikipelekwa na maji na wananchi kuwa katika taharuki.

Hali ya mvua ilivyo katika eneo la TAZARA Jijini Dar ambapo inajengwa Barabara ya juu (Flyover).

Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amefika katika eneo hilo na kushuhudia hali halisi, na kisha kutoa agizo kwa wakuu wa shule kuwa wanafunzi wapumzike nyumbani kwa siku mbili, mpaka hali itakapokuwa nzuri.

 

Aidha, Makonda amewaomba wakazi waishio maeneo hayo kuchukua tahadhari na kuondoka maeneo hayo kwa kipindi hiki cha mvua ili kuepusha madhara makubwa zaidi kuwatokea.

VIDEO: Mafuriko Jangwani, Hali ni Mbaya, Makonda Atinga Kushuhudia!

Loading...


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment