MAKONDA Azindua Huduma Mpya ya NHIF – VIDEO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amezindua huduma mpya kwenye mfuko wa bima ya Afya NHIF yenye lengo la kumpa nafasi ya kupata matibabu kwa urahisi kwa mkazi wa Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa Habari Makonda amesema huduma hii itamuhusu kila mwananchi anaeishi katika mkoa wa Dar es salaam ambapo kila mmoja atachangia 40,000 na kwa familia ya watu sita itachangia 150,000 kwa mwaka.

Aidha Makonda amewataka wananchi wa Dar es salaam kutumia fursa hiyo ili kuwarahisishia upatikanaji wa huduma ya matibabu na dawa.

Kwa upande mwingine Makonda amewataka wakazi wa Dar es salaam kujitokeza kwa wingi kesho katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kuipokea ndege ya pili aina ya Airbus A220-300 inayotarajiwa kuwasili majira ya saa 5.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment