The House of Favourite Newspapers

RC Makonda Awashtukia Wapigaji Dar, Awakabidhi Takukuru – Video

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  leo April 30,2019, amewashtukia baadhi ya wataalam wa masuala ya ujenzi wakiwemo makandarasi na washauri kwa kushindwa kusimamia vyema ujenzi wa miradi mbalimbali hasa ya barabara na kuongeza gharama za ujenzi.

 

“Wananchi wanahangaika na barabara wakati huu wa mvua, lakini sisi tunajilipa tu pesa za posho na mambo mengine, sasa naomba tuache mara moja.

 

“Nimekwenda Kigamboni wanajenga barabara wanaweka taa na mitaro tena imefunikwa kwa gharama ileile sawa na wilaya nyingine, inawezekana sisi hatujui, nyie wataalam mnafahamu zaidi.  Tumewaandikia barua Takukuru waje wakague, kwa nini gharama za ujenzi zinatofautiana tena pakubwa, wakati mkoa ni mmoja, urefu wa barabara ni uelule na mzigo unaopita kwenye barabara hizo ni uleule?

 

“Mnatumia vifungu mnakubaliana gharama ya mfereji Tsh milioni 300, halafu mkija kukaa tena mnaongeza, sasa tunawaomba Takukuru  watusaidie kuchunguza kwa nini pesa nyingi zinatumika, haya mambo ya utawala hapana, tunataka tujibane tupeleke kwenye ujenzi wa barabara nyingine kama Rais Magufuli anayofanya,” amesema Makonda.

 

Aidha, Makonda amekataza utaratibu wa kila mradi mkubwa kupewa wageni ambao hata wao wamekuwa hawafanyi badala yake wanakodi makampuni mengine ambayo yanajenga. Amesema kuwanyima fursa wazawa ni kuwafanya washindwe kukuza makampuni ya ndani hivyo kuwadidimiza.

 

Makonda ameagiza kuwepo na mkakati wa kuinua makampuni ya uejnzi ya wazawa na hata kama atapewa mgeni basi angalau asilimia 40 ya kazi hiyo ifanywe na mzaa na asilimia 60 ifanywe na mgeni na kuongeza kuwa miradi hiyo lazima ijenge uwzo wa kiuchumi wa mzawa.

VIDEO: MSIKIE MAGUFULI AKIZUNGUMZA

Comments are closed.