The House of Favourite Newspapers

Naibu Waziri Mkuu Dkt. Biteko Aongoza Mazishi ya Mkurugenzi wa TANESCO – Video

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko aongoza Mazishi ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Mhandisi Boniface Gissima Nyamo-Hanga katika Kijiji cha Migungani Wilaya ya Bunda mkoani Mara.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akiwasili katika Kijiji cha Migungani Wilaya ya Bunda mkoani Mara kwa ajili ya kushiriki Ibada ya Mazishi ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Mhandisi Boniface Gissima Nyamo-Hanga. Ibada hiyo inafanyika leo Aprili 16, 2025
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akisaini kitabu cha maombolezo katika Msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Mhandisi Boniface Gissima Nyamo-Hanga.
Sehemu ya waombolezaji katika Ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) Mhandisi Boniface Gissima Nyamo-Hanga, katika Kijiji cha Migungani Wilaya ya Bunda mkoani Mara Aprili 16, 2025