The House of Favourite Newspapers

Miili ya Watanzania 13 Waliofariki Ajalini Uganda Yaagwa Lugalo

0
Majeneza yenye miili ya marehemu.

MIILI ya Watanzania 13 ambao ni ndugu wa familia moja waliofariki kwenye ajali mbaya ya gari iliyotokea nchini Uganda hivi karibuni, imeagwa kwenye Hospitali ya Jeshi la Wananchi ya Lugalo jijini Dar es Salaam na baadaye kusafirishwa kuelekea Arusha, Kilimanjaro na Mpwapwa kwa ajili ya mazishi.

Waombolezaji wakati wa shughuli ya kuaga marehemu.

Katika shughuli hizo za kuwaaga marehemu, viongozi kadhaa wa serikali walikuwepo wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala na Utumishi), Angela Kairuki, Charles John Mwijage, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Waziri Maalum wa Kusimamia Jiji la Kampala, Betty Kamya kutoka Uganda aliyemwakilisha Rais Yoweri Museveni kukabidhi miili ya marehemu kwa ndugu zao.

Miili ya Marehemu ikipelekwa eneo maalum kwa ajili ya kuagwa.

Rais Museven ametuma salamu maalum za rambirambi ambazo zilisomwa na Betty kwa niaba yake na kupokelewa na Waziri Kairuki kwa niaba ya Rais Magufuli.

VIDEO YA TUKIO HILO

Leave A Reply