The House of Favourite Newspapers

LIVE: Miili ya Wanajeshi Waliouawa DRC Yarejeshwa Nchini

Miili ya wanajeshi hao ikishushwa kwenye ndege.

MIILI ya Askari 14 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliouawa na waasi wakilinda amani katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imewasili nchini leo, Jumatatu, Desemba 11,2017 saa 12 jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam.

 

Miili ya askari hao ikipelekwa kwenye gari ili kwenda kuhifadhiwa hospitali.

Miili hiyo imepokelewa na wanajeshi wenzao, ndugu, marafiki, jamaa na mamia ya wananchi waliojitokeza katika Uwanja huo jioni hii ambapo itaagwa Alhamisi, Disemba 14 katika Viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

 

Miili ikipelekwa kwenye gari.

Miili hiyo imesafirishwa kwa ndege za Umoja wa Mataifa kutoka nchini DR Congo.

Wanajeshi hao waliuawa wakati wa shambulio lililotekelezwa Alhamisi jioni kwenye kambi ya jeshi ya Semuliki eneo la Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini ambapo wanajeshi wengine zaidi ya 50 walijeruhiwa.

Askari wakibeba miili ya askari wenzao.

Umoja wa Mataifa ulisema wanajeshi 5 wa jeshi la DR Congo (FARDC) waliuawa pia kwenye shambulio hilo. Waasi wa ADF ndio wanaotuhumiwa kutekeleza shambulio hilo.

Miili hiyo imepokelewa na Wziri wa Ulinzi na JKT, Dk Hussein Mwinyi na Mkuu wa Majeshi, Venance Mabeyo.

Ndege ya UN iliyokuwa imebeba miili hiyo.
Maofisa wa JWTZ waliofika kupokea miili hiyo.

 

Comments are closed.