The House of Favourite Newspapers

Dkt Abbas: Kila Alichokiahidi JPM Amekitimiza – Video

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas leo Novemba 6, 2019 anaongea na wanahabari juu ya tathmini ya miaka minne ya Rais Magufuli katika ukumbi wa Maelezo jijini Dar es Salaam.

 

Akiongea na wanahabari haya ni baadhi ya vitu alivyovisema:-

“Tarehe 7 na 8 Novemba 2019 nchi yetu itakuwa mwenyeji wa mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na NORDIC. Katika kipindi cha miaka minne tumefuata utawala wa Sheria kwa kiasi kikubwa, sisi tumeendelea na tutaendelea kutekeleza wajibu wetu.

 

“Serikali ya awamu ya tano ni Serikali inayotatua changamoto za watanzania pamoja na kutekeleza miradi mikubwa ya kimaendeleo. Mafanikio haya ni siri ambazo siwezi sema ni mpya, ila ni dhamira ya nchi hii tangu uhuru wa kuwa na nchi inayojitegemea, kupinga vita rushwa, sisi awamu ya tano tulichokifanya ni kuongeza kasi katika hayo.

“Kila alichokiahidi kwenye kampeni Mhe. Rais Magufuli amejitahidi kutekeleza katika sekta mbalimbali nyingine ni mchakato zinaendelea kutekelezwa taratibu, kila utakapogusa kuna kitu kimefanyika kubadili maisha ya watanzania.

 

“Kila ambacho tumekifanya si kwa manufaa ya viongozi wa Serikali, ni kwa ajili ya watanzania, ni muhimu kwa kila mtanzania kulinda miradi yote inayotekelezwa na Serikali. Katika kipindi cha miaka minne madarasa zaidi ya 3000 yamekarabatiwa na kujengwa, tumejenga mabweni zaidi ya 500 katika vyuo vyetu, shule kongwe zaidi ya 65 zimekarabatiwa na imetumika zaidi ya Tsh. bil. 70.

 

“Mlinzi wa Miradi ya maendeleo ni kila mtanzania, miradi hii inatekelezwa kwa pesa za kodi watanzania, tuilinde. Katika kipindi cha miaka minne tumeongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba kutoka Tsh. Bil 31 mpaka Tsh Bil. 270, miaka hii minne tumeamua kuwekeza katika sekta ya afya, Tanzania sasa ni ‘Donor Country’ katika sekta ya afya,” amesema Abbas.

Comments are closed.