MWILI WA DKT. MENGI WAAGWA KARIMJEE – VIDEO

MWILI wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Media, Reginald Mengi, umeagwa leo Mei 7, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais John Magufuli na Makamu wake, Samia Suluhu wameungana na familia ya marehemu na waombolezaji wote kuuga mwili huo.

Baada ya kuagwa utasafirishwa kesho kwenda kijijini kwao Machame mkoani Kilimanjaro ambako utazikwa siku ya Alhamisi.

Tazama Mwili wa Mengi ukiagwa


Comments are closed.