Kartra

Mzee Mpili: Hii ni Zawadi ya Haji Manara – Video

SHABIKI maarufu wa Klabu ya Yanga, Mzee Haji Omari maarufu kama ‘Mzee Mpili’ amempa zawadi ya tisheti Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara ikiwa ni shukrani baada ya kumtimizia ahadi yake ya Tsh milioni 1.

 

Mzee Mpili amesema hayo leo Julai 15, mbele ya vyombo vya habari wakati akizindua Brandi yake ya ‘Sisi Tuna Watu’ ambapo atakuwa akiuza tisheti ni vitu vingine.

 

“Hii tisheti nimempa mjukuu wangu Haji Manara, amenifanyia mambo makubwa, amenipeleka mpaka kwake, kwa hiyo nimeona nimkirimia tisheti hii yenye rangi ya Simba (nyekundu).”

 

Kuna tisheti za rangi mbalimbali hasa Kijani na Njano ambazo tumetengeneza, lakini nyekundu hii moja tu ya Haji Manara, Mimi sitengenezi ya Simba, miiko yetu hairuhusu.

 


Toa comment