The House of Favourite Newspapers

LIVE: HOTUBA YA ODINGA BAADA YA UCHAGUZI KUFUTWA

0
Raila Odinga akizungumza na wafuasi wake.

Kiongozi wa Upinzani Kenya Raila Odinga amesema uamuzi wa mahakama wa kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais yanaashiria mwanzo wa Kenya mpya huku akieleza kuwa majaji walionyesha kwamba mahakama zinaweza kuwa na uhuru na kusimama dhidi ya nguvu za marais Afrika.

Odinga amedai kuwa tume ya uchaguzi nchini Kenya “imeoza” huku akisema maafisa wengi wakuu wa tume hiyo walikula njama kufanikisha wizi wa uchaguzi wa urais.

Odinga amesema ni lazima viongozi waliohusika wawajibishwe na kusisitiza kwamba mitambo ya tume ya uchaguzi ni lazima iwekwe wazi kwa ukaguzi.

Hayo yamejiri baada ya Mahakama yaKuu nchini humo kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa mwezi jana na kuagiza uchaguzi mpya uandaliwe katika muda wa siku 60.

Rais Uhuru Kenyatta amesema anatofautiana na uamuzi huo wa mahakama lakini anaukubali.

Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo akiwa na kura 8,203,290 (54.27%)

LIVE: HOTUBA YA ODINGA BAADA YA UCHAGUZI KUFUTWA

Global Tv Kenya: Mahakama Kuu Kenya Yafuta Matokeo ya Urais, Yaamuru Urudiwe

Leave A Reply