Rais Dkt. Samia Azindua Tume Ya Rais Ya Marekebisho Ya Kodi Ikulu, Dar – (Picha +Video)

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 4, 2024 akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi Dar es Salaam Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais Samia Suluhu amesema bado kuna malalamiko kutoka kwa Wafanyabiashara wanaolalamikia weledi kutozingatiwa wakati wa kukusanya kodi ikiwemo matumizi ya nguvu, lugha zisizo na staha na ubabe kwa baadhi ya Watumishi wa Serikali wanaohusika na utozaji kodi.
“Baadhi ya Wafanyabiashara wanalalamikia wingi wa kodi na tozo lakini pia viwango vya kodi kutokuwa rafiki na hii ni kawaida, unajua Mtu ana hiyari kwenda kulipa faini bila kulazimishwa mwenyewe kwasababu faini ni kodi inayotokana na kosa, kwahiyo Mtu analipa ili asiende Jela lakini kodi tunayoizungumzia hapa ni kodi inayotokana na kitu kizuri” amesema Rais Samia akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi.

