The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Rais Magufuli Afukunyua Madudu ya Mamlaka Maji Safi – Pwani

0

 

PWANI: Rais Magufuli amezindua rasmi mradi wa kusafirisha maji wa Ruvu Juu, Pwani ikiwa ni siku ya pili ya ziara ya siku tatu mkoani humo. Mradi huo utasaidia kupatikana maji Dar.

 

Aidha Rais Magufuli amemtaka Waziri wa Maji, kukomesha tatizo la kutoza wateja bili feki za maji, kuunganisha maji kwenye viwanda na kampuni bila kulipia bili, wafanyakazi wa Dawasa na Dawasco kupokea pesa za bili za maji kwenye akaunti zao binafsi.

 

Pia Rais, amemtaka Mkurugenzi wa Dawasa, Archard Mutalemwa kujiandaa kustaafu kwa heshima kwa sababu ameitumikia serikali kwa muda mrefu sana pamoja na kufanya mambo mengi kwa serikali za awamu zote. Amemtaka awaachie vijana waendeleze kuchapa kazi.

 

Sambamba na hayo, rais pia amezitaka taasisi za serikali kuhakikisha wanalipa bili za umeme vinginevyo wakatiwe umeme. amesisitiza kila mamlaka itimize wajibu wake.

 

Rais amemuagiza Waziri wa Maji, Gerson Lwenge kuhakikisha mradi wa maji wa Ng’apa- Lindi, unakamilika haraka, ikiwezekana waziri ahamie hukohuko.

VIDEO: MSIKILIZE RAIS AKIFUNGUKA

Leave A Reply