The House of Favourite Newspapers

Serikali Yafikia Maridhiano na Barric, Kugawana Makinikia 50 kwa 50 – Video

0

RAIS John Magufuli amepokea taarifa ya maridhiano kati ya serikali ya Tanzania na Kampuni ya uchimbaji madini ya Barric Ikulu jijini Dar es Salaam.

Akiwasilisha taarifa hiyo kwa Rais Magufuli, Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Paramagamba Aidan Kabudi amesema kuwa serikali na Barric wamefikia maridhiano mazuri na timu ya Barric iliyokuwa ikiongozwa na Mwenyekiti wake, John L. Thornton.

“Nadhani hata wao wameamini kuwa tuna uwezo mkubwa wa kuingia katika maridhiano na kufikia makubaliano makubwa, tofauti na ambavyo tungeazima wataalam wa nje kuja kufanya majadiliano hayo kwa niaba yetu, heshima yetu ingeshuka.

“Barric wamependekeza tutumie mfumo wa gawio la 50 kwa 50 ambao ni mfumo wa karne ya 21, jambo ambalo litakuwa na manufaa kwa taifa letu. Tunakupongeza Mhe. Rais kwa kuchukua hatua kulinda Rasilimali za nchi. Hatimaye hatua hizo zimeanza kuzaa matunda.

“Serikali itakuwa na umiliki wa madini mengine yatakayopatikana kwenye makinikia na wao kubaki na fedha, dhahabu na shaba. Kampuni ya Barrick imekubali kulipa kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 300 kwa ajili ya kukuza Uaminifu,” alisema Kabudi.

Naye rais Magufuli baada ya kupokea taarifa hiyo alikuwa na haya ya kusema.

“Nchi yetu ni tajiri, tumekuwa tukidhurumiwa sana. Huu ni mwanzo wa tu kwa Watanzania, bado tutaongeza nguvu katika kulinda rasilimali zetu. Nina uhakika jambo hili la 50 kwa 50 halijawahi kufanyika duniani kote Naamini mataifa mengine yatakuja kujifunza kwetu. Sasa hivi Barric Gold Cooperations ni ndugu zetu.

“Naomba mkae mfanye majadiliano na makampuni ya almasi na Tanzanite, atakayekataa basi aachane na sisi, tusifanye naye biashara na aondoke. Baada ya Tume hii ya dhahabu, naomba mkafanye ‘negotiation’ hii hii kwenye Almasi na Tanzanite. Wasipotaka waondoke!
“Ndio maana baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo ya maridhiano na Barric tulkiwaficha na tutaendelea kuwaficha ili kuzuia mambo ya rushwa,” alisema Magufuli.

Leave A Reply