LIVE: Rais MAGUFULI Awasili MALAWI kwa Ziara – Video

 

Rais Dk. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli tayari wameshawasili nchini Malawi kwa ziara rasmi ya Kiserikali ya siku mbili na kupokelewa na mwenyeji wao Rais wa Jamhuri ya Malawi, Arthur Peter Mutharika na mkewe, Bi. Gertrude Maseko.

Magufuli amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu, Mji wa Lilongwe nchini humo kwa ndege ya ATCL. Malawi ni nchi ya kwanza kuitembelea Kusini mwa Afrika tangu aingie madarakani.

Baada ya kurejea nchini ataanza ziara ya kikazi ya siku nane Mkoani Mbeya.

TAZAMA TUKIO HILO HAPA

Loading...

Toa comment