Video: Rais Samia Awasili Ikulu Kenya, Rais Kenyatta Ampokea

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Mei 04, 2021 ameanza ziara ya siku mbili nchini Kenya ambapo mbali na kufanya shughuli mbalimbali akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, lakini pia atalihutubia Bunge la Kenya.

 

Ziara hii ya rais Samia ni muendelezo wa jitihada za nchi hizo mbili kuboresha na kuendeleza uhusiano wa muda mrefu na itakuwa ndio ziara ya pili nje ya taifa lake kwa rais Samia tangu alipochukua madaraka kutoka kwa hayati Dkt John Magufuli.

 

Rais Samia anatarajia atafanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Uhuru Kenyatta kisha atalihutubia Bunge la Kenya litakalojumuisha Wabunge wa Mabunge yote mawili.

Aidha, Rais Samia atahudhuria na kuhutubia mkutano wa jukwaa la wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania utakaofanyika jijini Nairobi.

 

Alifanya safari yake ya kwanza akiwa Rais nchini Uganda mnamo Aprili 11 na Rais Yoweri Museveni akielezea kuwa lengo la ziara yake ni kuimarisha uhusiano wa nchi mbili na kumaliza makubaliano ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka nchini Uganda.

 

Rais huyo ameonekana kutopendelea kulinganishwa na Magufuli na amewashutumu wabunge wa Tanzania kwa kufanya hivyo.

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCxTecno


Toa comment