The House of Favourite Newspapers

Makonda: Marufuku Watendaji Wa Dar Kutoka Nje Ya Mkoa

0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiongea na watendaji wake.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo amepiga marufuku watendaji wa serikali wa mkoa huo kutoka nje ya mkoa bila kutoa taarifa kwake. Makonda amepiga marufuku hiyo wakati wa kongamano la tathimini ya hali ya miundombinu ya barabara za mkoa huo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Posta jijini Dar.

Watendaji mbalimbali wakiendelea kumsikiliza Makonda.

Kauli hiyo ya Makonda imekuja baada kukosekana kwa watendaji ambao walitakiwa kuhudhuria kongamano hilo kwa madai kuwa wako nje ya mkoa kikazi huku waliobakia wakishindwa kueleza kuwa wapo kwa ajili ya kazi gani.

…Akiendelea kuongea nao.

” Kuanzia sasa hakuna mtumishi wa mkoa huu kutoka nje bila kutoa taarifa hata kama ni kazi ya wizara gani lazima mtoe taarifa, kumekuwa na tabia ya watu kujitengenezea tu safari ambazo hazijulikani wakati hata rais wetu alishazikataza,” alisema Makonda.

(PICHA: DENIS MTIMA/GPL)

 

VIDEO: Mshuhudie Paul Makonda Uone Kitakachotokea Hapa!

Leave A Reply