ABBAS: RAIS MAGUFULI HAKUTOA AHADI YA KUONGEZA MISHAHARA – VIDEO

Mkurugenzi Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr Hassan Abbas, amefafanua kwamba Rais John Magufuli hakuzungumzia masuala ya wafanyakazi wote walioko kwenye utumishi wa umma kuhusu kuongeza mishahara.

Abbas alisisitiza kwamba alichokikataa Rais ni hoja ya madiwani kutaka kuongezwa posho yao kutoka 350,000/= hadi 800,000/=, kiwango ambacho ni zaidi ya asilimia 150 na zaidi.

Aliyasema hayo kufuatia kauli za chama cha wafanyakazi nchini (TUCTA) na vyama vingine vya siasa kwamba Rais Magufuli alikuwa amekiuka ahadi yake kwamba angeongeza mishahara ya wafanyakazi serikalini na katika sekta ya umma nchini.

Loading...

Toa comment