The House of Favourite Newspapers

Video + Pichaz: SportPesa Waingia Mkataba wa Kuidhamini Singida United

0

Mkurugenzi Mkuu wa SportPesa,Pavel Slavkov,(kulia), akimpongeza Mratibu Mkuu wa Singida United, Festo Sanga, wakati wa makabidhiano ya nyaraka za mkataba mpya.

Hatimaye Klabu ya Singida United ya mjini Singida, mapema leo imeingia mkataba wa udhamini wa zaidi ya shilingi Mil. 300, ambao utadumu ndani ya mwaka mmoja na Kampuni ya Mchezo wa Kubahatisha ya SportPesa.

Waandishi wa habari (kushoto), wakifuatilia kikao cha kusaini mkataba huo ndani ya Hyatt Hoteli Posta jijini Dar, mapema leo.

Makubalino hayo ambayo yamefanyika ndani ya Hoteli ya Hyatt Posta jijini Dar es Salaam na kusainiwa chini ya Mkurugenzi wa SportPesa Pavel Slavkov na Katibu Mkuu wa Singida United Abdulrahmani Sima.

 

Nahoza wa Singida United, Niza Halfan (kulia), akipokea jezi itakayotumia timu hiyo kwenye msimu huu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa SportPesa, Pavel Slavkov wakati wa kuasiniana mkataba huo.

Leave A Reply