The House of Favourite Newspapers

FT: Tanzania 2-0 Malawi – Uwanja Wa Mkapa, Mechi Ya Kirafiki

0

TIMU ya taifa ya Tanzania leo Juni 13 imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Malawi katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote ambapo ilikuwa ngumu kipindi cha kwanza kwa ngome za timu zote kuokota mpira nyavuni.

 

Dakika ya 68 nahodha wa Stars, John Bocco alipachika bao la kwanza ambalo liliwanyanyua mashabiki kwa furaha.

Iliwachukua dakika 7 Stars kuandika bao la pili ambapo mtupiaji alikuwa ni Israel Patric ambaye alipiga pigo huru kiufundi likazama mazima nyavuni na kumuacha kipa wa Malawi akiwa hana la kufanya.

 

Ilikuwa ni dakika ya 75 baada ya Kibu Denis kufanyiwa madhambi nje kidogo ya 18 jambo ambalo liliwafanya Malawi washindwe kuwa na namna ya kupindua meza kwa dakika ambazo zilibaki.

 

Mpaka dakika 90 zinakamilika ubao wa Uwanja wa Mkapa ulikuwa unasoma kwamba Tanzania 2-0 Malawi.

 

Leave A Reply