The House of Favourite Newspapers

FT: TOWNSHIP ROLLERS 0-0 YOUNG AFRICANS, KUTOKA BOTSWANA

MPIRA UMEKWISHA

Dk 91, Ajib na mpira, anapiga chenga mabeki wa Rollers, anadonoa shuti lakini mabeki wanaokoa

DAKIKA 90 ZIMEKAMILIKA

Dk 86, Nsanjigwa ametolewa nje baada ya kuanza kubishana na Mwamuzi, ameenda jukwaani.Dk ya 85, Dakika 5 zimesalia mpira kumalizika, milango bado ni migumu.
Dk 83, Ajib anafanywa faulo, inapigwa sasa kuelekea Rollers, upande wa kulia mwa Uwanja

Dk 83, Ajib anafanywa faulo, inapigwa sasa kuelekea Rollers, upande wa kulia mwa Uwanja

82, Rostand anafanya kazi kubwa leo, anaokoa krosi hapa, kona nyingine.

Dk 75, Faulo, Chirwa anapewa kadi ya njano baada ya kucheza madhambi.

Dk 70, Bado Rollers wameliandama vilivyo lango la Yanga.
Dk 68, Inapigwa, Dante anaokoa kwa Kicgwa, Yanga wanafanya mabadiliko. Yusuph Mhilu anatoka na Mwashiuya anachukua nafasi yake.
Dk 67, Kona nyingine inapigwa kuelekea Yanga

Dk 62, Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Kamusoko, anaingia Ajibu
Dk 59, Yanga wanapandisha mashambulizi sasa lakini Rollers wanaokoa, wanakwenda langoni mwa Yanga, linapigwa shuti kali, Rostand anaokoa kwa kupiga shuti kueleka kwa wapinzani.

Dk ya 54, Inapigwa huku, kipa anadaka.
Dk 53, Hatariii, shuti kali linapigwa na mshambuliaji wa Rollers, Rostand anaupangua mpira na kutoka nje, kona.

Dak 49, Hatari langoni mwa Yanga ndani ya penati boksi, Rostand anaokoa.
Dk 48, Rollers wanapandisha mashambulizi, Gadiel Michael anatoa mpira, unarushwa kuelekea Yanga, unamkuta lemponye, anapiga, Dante anaokoa.
Dk 46, Mpira umesimama, mchezaji wa Township ameumia, unapigwa kuelekea Yanga
Dk 45, Yanga wanaanzisha, matokeo ni 0-0.

DAKIKA 45 ZA KIPINDI CHA PILI ZIMEANZA

DAKIKA 45 ZA KWANZA ZIMEMALIZIKA, MPIRA NI MAPUMZIKO

Dk 45, Matokeo ni 0-0 bado
Dk 44, Rollers wanakwenda sasa, wanashambulia kueleka lango la Yanga, wanapotezana hapa, Yondani anaokoa mpira na kupiga mbele.
Dk 43, Papy amelala chini, yawezekana akawa ameumia, madaktari wanaingia kumpa huduma.

Dk ya 34, Obrey Chirwa yupo chini, mpira umesimama, Lwandamina anajibizana na, Yondani anaingilia anapewa kadi ya njano.
Dk 33, Juma Abdul anautoa mpira nje, Rollers wanarusha, hatari katika eneo la Yanga ndani ya penati boksi, wanarudisha tena nyuma na kuanza upya.
Dk 32, Inapigwa unamkuta huku Mhilu, anapiga shuti lakini inakuwa goli kiki.
Dk 31, Mpira unarushwa kuelekea Yanga, Yanga wanauchukua, kwake Chirwa, faulo, inapigwa kuelekea Rollers.

Dk ya 28, Makapu analambwa kadi ya njano baada ya kucheza faulo, inapigwaaa, hatari, Mwamuzi anasema offside.

Dk 27, 0-0 mpaka sasa, kila timu inapambana kupata bao la mapema

Dk 22, Youthe Rostand ameumia, anapeana tano na Mwamuzi, tayari ashainuka

Dk 21, 0-0 mpaka sasa, kila timu inapambana kupata bao la mapema, Rollers wanakwenda, pigwa moja ndefuuu, inatoka, free kiki kuelekea Rollers.

Dk 17, Yusuph Mhilu anaenda na mpira sasa, anaukokota na anauota mwenyewe, unarushwa kuelekea Yanga

TUNAOMBA RADHI KUTOKANA NA MATANGAZO YA AZAM TV KUKATIKA, TUTAREJEA PALE WATAKAPOREJEA TENA HEWANI

Dk 5, Kapteni wa Township anapoteza pasi kati mwa uwanja baada ya kutenegezewa na mwenzake, mpira unakwenda nje, Yanga wanarusha
Dk 5, Mpira umeanza kwa kasi, kila timu inajaribu kutafuta bao la mapema
Dk 3, Township wanamiliki mpira eneo la kati, unapigwa kwenda mbele lakini unatok nje
Dk 2; Dakika ya pili ya mchezo, mpira umeanza punde

Comments are closed.