The House of Favourite Newspapers

FT: Mbao 1-0 Yanga Uwanja wa CCM Kirumba, Mbao Watinga Fainali

0

 

 

 

 

Kikosi cha timu ya Yanga.

Dakika ya 96: Mchezo bado unaendelea kwa kasi.

Dakika ya 95: Mbao wanafanya mabadiliko.

Dakika ya 94: Mbao wanafanya shambulizi kali langoni kwa Yanga lakini mpira unaondolewa na walinzi wa Yanga.

Dakika ya 86: Mpira umekuwa ukichezwa zaidi mbele ya lango la Mbao FC, Yanga wanapata faulo nje kidogo ya lango la Mbao FC kutoka upande wa kulia.

Dakika ya 83: Obrey Chirwa wa Yanga anatoka, nafasi yake inachukuliwa na Emmanuel Martine.

Dakika ya 80: Kona inapigwa, Yanga wanakosa nafasi ya wazi baada ya mpira wa kichwa wa Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kuokolewa na kipa kuwa kona tena ambayo inapigwa lakini mabeki wa Mbao wanaokoa.

Dakika ya 72: Yanga wanapata faulo nje kidogo ya eneo la 18 la Mbao FC, wakati huohuo Mbao wanafanya mabadiliko, anatoka Bernard ambaye alipata njano muda mfupi uliopita anaingia Ndaki Robert.

Dakika ya 68: Mashabiki wa Mbao wengi wao wakiwa na jezi nyekundu wanashangilia kwa nguvu na kuimba nyimbo za vijembe kwa wapinzani wao.

Dakika ya 67: Yanga wanamtoa Hassan Kessy, anaingia Juma Abdul.

Dakika ya 60: Mchezo umekuwa na kasi kubwa, Yanga wanamiliki mpira muda mwingi, mchezo unachezwa zaidi kuanzia katikati kueleke kwenye lango la Mbao.

Dakika ya 51: Haruna Niyonzima yupo chini baada ya kuchezewa faulo na kiungo wa Mbao, Hatuna anamlalamikia mwamuzi kuwa kwa nini hakumpa kadi mpinzani wake.

Dakika ya 46: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Said Juma Makapu, anaingia Geofrey Mwashiuiya.

Kipindi cha pili kimeanza hapa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, ni mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA na Mbao wapo mbele kwa bao 1-0.

Timu zimesharejea uwanjani. Mbao FC wamepiga magoti wansali kwa pamoja, kisha wanaelekea kujipanga kuanza mchezo.

Dakika ya 50: Mwamuzi anapuliza filimbi kukamilisha kipindi cha kwanza,

Dakika ya 48: Mchezo unaendelea, muda wowote wataenda mapumziko,

Dakika ya 46: Yanga wameongeza presha kubwa, kipa wa Mbao FC analala chini, mwamuzi anasimamisha mchezo kutuhusu apatiwe matibabbu.

Dakika ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika mbili za nyongeza.

Dakika ya 44: Haruna Niyonzima wa Yanga anapiga shuti kali linapaa juu ya kango,

Dakika ya 41: Straika wa Yanga, Amiss Tambwe anapata nafasi ya kuruka kichwa, anapiga mpira unatoka nje ya lango kidogo.

Dakika ya 40: Kocha Mkuu wa Yanga,George Lwandamina anasimama kutoa maelekezo kwa wachezaji wake,

Dakika ya 37: Haji Mwinyi wa Yanga anaambaa na mpira kushoto mwa uwanja, anabanwa, mpira unatoka unakuwa goal kick.

Dakika ya 30: Kasi yua mchezo imeongezeka kutokana na Mbao kuongeza kasi huku Yanga wakuonekana kujipanga taratibu.

Dakika ya 27: Mbao wanapata bao la kwanza baada ya beki wa Yanga, Andrew Vicent ‘Dante kujifunga wakati akiokoa mpira wa krosi, Mbao walicheza vizuri kuanzia katikati ya uwanja kisha kupiga krosi ambayo ilimbabatiza Dante na kujaa wavuni.

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dakika y 25: Mchezaji wa Mbao anaotea ikiwa ni mara yao ya tano katika mchezo huu.

Dakika ya 23: kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko anapiga shuti kali langoni kwa Mbao FC linadakwa/

Dakika ya 22: Mbao wanaonyesha ufundi na wanamiliki kiungo kwa kupiga pasi za uhakika, wanashangiliwa kwa nguvu.

Dakika ya 18: Mchezo unachezwa zaidi katikati ya uwanja, Mbao wanapata nafasi ya kupiga shuti linalotoka juu kidogo ya lango la Yanga.

Dakika ya 15: Beki wa Yanga, Hassan Kessy anapanda na mpira, anapiga krosi ambayo inazuiwa na mabeki wa Mbao.

Dakika ya 12: Mbao wanacheza counter attack lakini wanashindwa kuwa na mpango mzuri, mpira unatoka nje unakuwa wa kurushwa.

Dakika ya 11: Yanga wanatulia na kumiliki mpira muda mwingi lakini hawajafika langoni mwa Mbao kwa kufanya mashambulizi ya nguvu.

Dakika ya 8: Mbao wanafika langoni mwa Yanga mara mbili, mara zote hawajawa na madhara.

Kikosi cha Mbao FC

Dakika ya 4: Straika wa Yanga, Obrey Chirwayupo chini, amelala mwenyewe, inaonekana ana maumivu ya msuli. Mchezo umesimama kwa muda kisha ukaendelea baada ya Chirwa kupatiwa matibabu na kurejea uwanjani

Dakika ya 3: Mchezo bado haujawa na kasi, timu zote zinasomana.

Idadi ya mashabiki ni wengi japokuwa hawajajaa uwanjani kote. Kelele ni nyingi pia za mashabiki.

Dakika ya kwanza: mwamuzi ameanzisha mchezo rasmi.

Timu zote zimeshaingia uwanjani, mchezo utaanza muda wowote kutoka sasa.

Mbao FC ya Mwanza inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Yanga katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho maarufu kwa jina la FA, kuanzia saa 10 jioni, leo Jumapili

Kikosi cha Yanga SC leo dhidi ya Mbao FC

1. Deogratius Munishi

2. Hassan Kessy

3. Haji Mwinyi

4. Vicent Andrew

5. Nadir Haroub

6. Juma Saidi

7. Simoni Msuva

8. Thabani Kamusoko

9. Obrey Chirwa

10. Amissi Tambwe

11. Haruna Niyonzima

 

Akiba

Beno Kakolanya

Oscar Joshua

Juma Abdul

Juma Mahadhi

Emanuel Martin

Geofrey mwashuiya

Deusi Kaseke

Leave A Reply