The House of Favourite Newspapers

Video: Donald Trump Aapishwa Kuwa Rais wa 45 wa Marekani (+Pichaz 40) za Matukio

 trump24

WASHNGTON DC, MAREKANI: Mfanyabiashara Maarufu duniani, Donald John Trump ameapishwa rasmi kuwa Rais wa 45 wa Marekani huku bwana Mike Pence akiapishwa kuwa Makamu wa Rais wa nchi hiyo, tukio lililofanyika mnamo majira ya saa 6:00 mchana kwa saa za Amerika ya Kaskazini sawa na saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

trump25

Trump akiapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani.

 trump-pence

Mike Pence akiapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Marekani.

trump-7

Donald Trump na mkewe Melania Trump walianzia katika ibada ya Misa kwenye Kanisa la St. John’s amjira ya saa mbili asubuhi na baadaye kuelekea Ikulu ya Marekani ambako walipokelewa na mwenyeji wao Rais aliyemaliza muda wake, Barack Obama na Mke wake, Michele Obama kabla ya kuelekea kwenye Jengo la Bunge ambapo shughuli ya kuapishwa imefanyika.

trump2

trump23Trump akihutubia mara baada ya kuapishwa.

Katika hotuba yake mara baada ya kuapishwa, Trump ameahidi kuilinda miapaka yote ya Marekani huku akieleza kuwa nchi hiyo imekuwa ikifanya juhudi kubwa kulinda mipaka ya nchi nyingine na kusahau mipaka yake hivyo kuingiliwa na wabaya wao na kusababisha maafa makubwa kwa Wamarekani.

trump3

Aidha Trump amewataka Wamarekani wawe wamoja ili waweze kushirikiana kuirudisha hadhi ya nchi hiyo kwa kutumia kauli mbiu yake ya #MakeAmericaGreatAgain.

trump4Donald Trump ameapishwa kwa Biblia mbili, moja ni ile aliyokabidhiwa na mama yake na nyingine iliyotumiwa na Abraham Lincoln ambaye ni muasisi wa Demokrasia.

trump27

Donald Trump ameahidi kuwaunganisha Wamarekani alipokuwa anawahutubia wafuasi wake wakati wa tamasha la mkesha wa kuapishwa kwake kuwa rais.

Akiongea katika vidato vya sanamu ya ukumbusho wa Lincoln mjini Washington DC, rais huyo mteule pia aliahidi kuleta mabadiliko.

 

trump-melania

Miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo iliyodumu saa mbili ni mke na watoto wake, mwigizaji Jon Voight na mwanamuziki aliyeimba wimbo wa Soul Man, Sam Moore.

Bw Trump baadaye aliweka shada la maua katika makaburi ya taifa ya Arlington, Virginia.

trump6

Trump akia akisalimiana na kasisi  Luis Leon kabla ya kuingia kanisani wakati alipoenda kwenye ibaada yna familia yake leo.

Hafla hiyo ya Make America Great Again! (Fanya Marekani kuwa kuu tena) ilikuwa wazi kwa umma kuhudhuria na miongoni mwa waliotumbuiza ni nyota wa muziki wa country Toby Keith na Lee Greenwood.

trump8 trump9

 

trump10 trump11 trump12 trump13 trump14

trump15 trump16 trump17 trump18 trump19 trump20 trump21

Comments are closed.