The House of Favourite Newspapers

Azam FC Yashinda Fainali Kombe la Mapinduzi, Yaichapa Simba SC Bao 1-0

azam-na-simba-1

Azam FC wameifunga Simba  SC kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, na kufanikiwa kutwaa Kombe la Mapinduzi kwa Mara ya 3 sasa.
Mfungaji Himid Mao dakika ya 13.

Dk 90+3, Mkude aanaachia mkwaju hapa, lakini Manula anadaka na kuinuka kwa mbwembwe kabisa

Dk 90+2, Stephan wa Azam FC yuko chini pale (jukwaani, mashabiki wa Simba wanaonekana kukata tamaa, wanaanza kuondoka)
DK 90+1 Dalili zinaonyesha Simba hawana nafasi tena kutokaba ba Azam FC kuanza kupoteza muda katika dakika za mwishoni. lakini hata wachezaji wa Simba wanaonekana kukata tamaa, mashabiki wao wanaanza kuondoka uwanjani.
azam-na-simba-3

DAKIKA 4 A NYONGEZA
Dk 88, Azam FC wanaokoa hapa na kuwa konaaaaa, inachongwa na Zimbwe lakini Manula anadaka kwa ustadi kabisa hapa
Dk 86, Kapombe analala na kuokoa mpira wa hatari langoni mwake, unakuwa wa kurusha
Dk 85, Simba wanagongenaa vizuri hapa, Mavugo anampa Pastory lakini Azam wanaokoa hapa
Dk 83, Manula yuko chini, hali inayoonyesha anataka kuanza kukata kasi ya mashambulizi ya Simba kwa kusingizia ugonjwaSUB: Dk 82, Azam wanamuingiza Enock Atta Agyei kuchukua nafasi ya Himid Mao aliyefunga bao pekee la Azam

Dk 78 mbele ya Banda, Bocco anajipinda na kuachia mkwaju hapa lakini gooal kick

SUB: Dk 76, Simba wanafanya mabadiliko tena hapa, Mnyate anaingia kuchukua nafasi ya Kichuya.

SUB: Dk 70, Simba wanafanya mabadiliko ya pili, Pastori Athanas anaingia kuchukua nafasi ya Mzamiru Yasin

azam-na-simba-4SUB: Dk 68, Azam wanamtoa Yahya Mohamed, nafasi yake inachukuliwa na Mudahdhir Yahya.

Dk 60, Gadel anafanya kosa hapa mpira unapitiwa, anapewa Mavugo lakini anaukosa mpira hapa
SUB Dk 57, Azam wanamuingiza Frank Domayo kuchukua nafasi ya Joseph Mahundi
Dk 51: Yakub anacheza mpira wa adhabu kuelekea lango la Simba, anapaisha.
KADI Dk 50, Banda analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Himid aliyekuwa anakwenda langoni kwao

azam-na-simba-5Dk 50, Azam FC wanajibu, shambulizi hapa, krosi ya Sure Boy lakini inakosa mtu
Dk 49, krosi nyingine ya Bukungu hapaaaa, Kichuya anapiga kichwa lakini umbo linakuwa tatizo kwake
Dk 48, krosi safi ya Bukungu inapita katikati ya lango la Azam
azam-na-simba-2Dk 47, Simba wanaonekana kufanya masihara hapa, mpira unamfikia Yahya hapa, lakini Mwanjale anajitokeza na kuokoa

Dk 45: Tayari Simba wamekwisha anza mpira pale kati kwa umaridadi mkubwa kabisa.

Timu zimerejea tena uwanjani kwa ajili ya kipindi cha pili cha dakika 45 za lala salama.
 azam-na-simba-6
Mpira ni mapumziko.
Dk 45+1: Himid Mao anapigwa kadi ya njano kwa kumkanyaga Bukungu tumboni akiwa chini.
Dakika 3 zimeongezwa kwenye kipindi hiki cha kwanza.
Dk 42: Simba wanafanya mabadiliko, Mwinyi Kazimoto anatoka na Laudit Mavugo anaingia, Simba wanaonekana kuimarisha safu ya ushambuliaji.
azam-na-simba-7Dk 33,  Aboubakar Salum anapewa kadi ya njano kwa kumuangusha Kotei lakini anamlaumu mwamuzi kwa kupuliza filimbi.
Dk 30, Simba wanaonekana kucheza zaidi na kusukuma mashambulizi mengi kulisakama lango la Azam FC mara kwa mara.
Dk 28, Banda anaachia shuti kali la mkwaju wa adhabu lakini Manula anaonyesha umahiri wa juu anapangua na kuwa kona, inachongwa na wachezaji Azam FC wanaokoa

azam-na-simba-8Dk 26, Krosi nyingine ya Zimbwe, Yakubu anaruka na kupiga kichwa, konaaa, inachongwa na Kotei lakini Azam wanaokoa.

Dk  25: Bukungu anaachia krosi nzuri Simba wanashindwa kumalizia.

Dk  19: Simba wanakosa bao, Kotei anachia fataki maridadi hapa, lakini mpira unapita juu ya lango la Azam

Dk  18: Bukungu anaingia kwenye 18 za lango Azama ancheza mkwju lakini golikipa Manura anakamata.

Dk 17: Mohammed Huseein anachezewa faulo.

Dk 16, Joseph Mahundi anataka kuondoka tena anaweka chini na Kichuya.

Dk 15: John Boko anakosa bao la wazi tena kwenye lango la Simba.

Dk 13: Gooooooooooooooooooooooooaaal, Himid Mao anaifungia Azam bao la kwanza kwa kupiga bonge la shuti.

Dk 10: John Boko anakosa bao kwenye lango la Simba.

Dk 10: Kotei anamminyia Kichuya anashindwa kumalizia na mabeki wa Azam wanaondoa mpira kwenye hatari.

Dk8: Himid Mao anamchezea madhazmbi Mwinyi kazimoto, faulo inapigwa kuelekea lango la Azam.

Dk4: Timu zote zinacheza kwa kuogopana, mpira unatoka nje kila mara.

Dk3: Bukungu anajaribu kuingia kwenye lango la Azam anashindwa, mpira unachezwa kwa umaridadi mkubwa.

Dk 2, Kichuya anatimua mbio kutoka katikati ya uwanja lakini Azam FC wanakuwa makini na kuondosha hatari ndani ya 18

Dk 1: Tayari Azam wameanza kugusa mpira katikati.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ndiye Mgeni rasmi kwenye mchhezo huo, anasalimiana na timu zote uwanjani.

Timu zinaingia uwanjani tayari.

Comments are closed.