The House of Favourite Newspapers

LIVE UPDATES: Simba 1 vs Yanga 1 Kutoka Uwanja Wa Taifa

Dakika ya 46 mpira umeanza, mabadiliko yanafanywa ambapo Kelvin Yondani anaenda benchi na nafasi yake kuchukuliwa na Dante.

Dakika ya 45 mwamuzi Martin Sanya anapiga filimbi kuashiria mpira ni mapumziko, Yanga 1 na Simba 0.

Dakika ya 44 Simba wanaongeza kujituma lakini shuti la Ibrahim Ajibu linatoka nje na kuwa Goal Kick.

Dakika ya 42 Simba wanapata kona baada ya shambulizi kali lililofanywa na Mavugo na kuokolewa na kipa wa Yanga. Kona inapigwa na Mohammed Hussein ‘Zimbwe’ na inatoka nje.

Dakika ya 44 Yanga wanajitahidi kukaba kwa staha huku wapinzani wao wakiwa na presha kubwa baada ya kufungwa goli na mchezaji wao kutolewa kwa kadi nyekundu.

Dakika ya 42 mchezaji wa Yanga Amiss Tambwe anafanyiwa madhambi na refa anampa kadi ya njano mchezaji wa Simba, Mzamiru.

Dakika ya 41 Yanga wanajibu shambulizi kupitia kwa Mahadhi.

Kichuya anafanya shambulizi lakini umakini unamnyima nafasi ya kuipa timu yake goli la kusawazisha.

Dakika ya 36 Donald Ngoma anapiga shuti kali linalodakwa na kipa Angban.

Dakika ya 35 timu ya Yanga wanafanya shambulizi, shuti la Mbuyu Twite linatoka nje.

Dakika ya 30 mpira unaendelea huku mchezaji wa Simba Jonas Mkude kapewa kadi nyekundu baada ya kumtolea maneno machafu mwamuzi.

Mpira umesimama Uwanja wa Taifa, baadhi ya mashabiki  wa Simba wanakimbia kutoka nje ya uwanja, viti vinaendelea kung’olewa upande waliokaa mashabiki wa Simba.

Dakika ya 26 Amis Tambwe anawainua mashabiki wa Yanga anafunga goli la kwanza.

Dakika ya 24 mchezaji Amis Tambwe anafanya faulo na mpira unapigwa kuelekea lango la timu ya Yanga, mpira unatoka nje.

Kelvin Yondani anaongoza ukuta wa Yanga unaokaba kwa kutumia nguvu na umakini, mchezo umejaa kila aina ya ufundi kutoka pande zote mbili.

Yanga wanacheza kwa umakini wa hali ya juu wakikaba kwa pamoja na wanaposhambulia wachezaji wote wanapanda kusaidia..

Dakika ya 16 Yanga wanajipanga na kuingia kwenye eneo la hatari kwa ushirikiano wa Tambwe, Ngoma, Mahadhi… Off side.

Dakika ya 13 shuti la Mavugo linatoka nje.

13Dakika ya 11 mchezaji wa Simba, Mavugo anafanyiwa rafu na kutolewa nje kutibiwa.

Dakika ya 09 Mavugo anapiga mpira wa faulo na kugonga ukuta wa mabeki wa Yanga.

Yanga wanapata kona ya kwanza kwa makosa ya beki.

Kikosi cha timu ya soka ya Simba wameanza kwa kasi kupitia kwa wachezaji wao Kichuya, Mavugo na ajibu bado timu zote zinaviziana.

Mpira umeanza saa kumi kamili. Timu ya Simba wakiwa wamevaa jezi zao za rangi nyekundu na Yanga wamevaa jezi za rangi ya kijani.

simba-2kikosi cha timu ya Simba.

yanga-fckikosi cha timu ya Yanga.

simbaViongozi Mbalimbali wakiwa tayari uwanjani kuangalia pambano hilo.

Comments are closed.