The House of Favourite Newspapers

Rais Magufuli Akizindua Ujenzi wa Maghorofa Magomeni Kota

0

Rais Magufuli akihutubia

Rais wa Jamhuri ya Serikali ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amezindua rasmi ujenzi wa majengo matano ya ghorofa 8 kila moja katika maeneo ya Magomeni Kota jijini Dar es Salaam.

Akizindua ujenzi huo ambao utagharimu takribani TZS bilioni 20, Rais Magufuli amesema kuwa majengo hayo yatakuwa na unafuu mkubwa kwa wakazi wa Dar, lakini pia ndani ya majengo hayo kutakuwa na maduka ambayo wafanyabiashara wataweza kuweka biashara zao hivyo hakuna ulazima wa mtu atakayeishi humo kutoka kwenda kufanya mahemezi nje.

Hizi ni baadhi ya kauli alizozizungumza Rais Magufuli wakati wa uzinduzi huo;

Wazee wangu wa Magomeni waliteseka sana, lakini naamini sasa mateso yao yanaelekea kuisha. Nafahamu mikoa mingi ina maeneo yaliyotengwa kwa makazi ya watu, lakini waliondolewa na watu wenye nguvu kwa hila.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria.

Nyumba hizi zitakapokamilika, wakazi 644 waliokuwa hapa awali, nilisema watakaa miaka mitano bure bila kulipa kodi.

Rais Magufuli alimpa wasaa Mbunge wa Kinondoni, Mtolea kuwasalimia wananchi.

Mtakapokuwa mnakaa bure kwa miaka mitano, ningependa muweke mikakati ya kumilikishwa kama alivyosema Waziri Lukuvi. Maeneo kama haya ya Magomeni Quarters yaliyopo sehemu nyingine nataka yawe chini yangu (serikali).

Haya majengo matano yenye ghorofa 8 kila moja yamegharimu TZS bilioni 20. Ukikuta jengo limejengwa kwa bilioni 200 ujue tumeibiwa.

Wasanii wakiwasili eneo hilo.

Ukikuta watu wanalalamika kwa jinsi tunavyobana matumizi ili kusaidia wananchi, nawaomba Watanzania muwapuuze wote.

Mzee Karume alijenga nyumba za wananchi wake kwenye miaka ya 1970. Haiwezekani sisi tunaotawala leo tushindwe kujenga.

Rais Magufuli alimpa mkazi mkongwe wa Magomeni Kota aweze kukata utepe wa kuzindua ujenzi huo.

Kikongwe huyo akifurahia baada ya kukata utepe.

Leave A Reply