The House of Favourite Newspapers
gunners X

LIVE: Uzinduzi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta Kutoka Uganda Hadi Tanga

0

 

Tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefika katika Viwanja vya Chongoleani jijini Tanga ambapo uzinduzi wa Ujenzi wa Mradi wa Mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Bandari ya Tanga utafanyika.

-Yupo pia Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu wa Tanzania Majaliwa Kasim Majaliwa, Mama Janeth Magufuli, Mama Maery Majaliwa.

-Wapo pia viongozi waandamizi wa serikali akiwemo Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Mwigulu, William Lukuvu, Makame Mbarawa, Hussein Mwinyi makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu pamoja na wakuu wa mikoa mbalimbali.

-Sasa Rais Magufuli anampokea Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni na tayari wote wawili wanaingia ukumbini.

-Mkuu wa Mkoa wa Tanga anatambulisha viongozi waliofika na kutoa salam kwa Marais wote wawili.

-Bomba litachukua mikoa 8, wilaya 24 na vijiji 124 ambapo wakandalasi watatu kutoka nje watasimamia-Naibu Waziri Medard Kalemani.

Leave A Reply