Breaking News: Wallace Karia Aibuka Mshindi Kiti cha Urais wa TFF

Kamati ya Uchaguzi ya TFF ikijiandaa kutangaza majina ya washindi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wakili Revocatus Kuuli amemtangaza Rasmi, Wallace Karia kuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania na Michael Wambura kuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo.

 

Baadhi ya wagombea wakisubili matokeo.

Wallace Karia ameibuka mshindi wa kiti hicho baada ya kuwaburuza wapinzani wake kwa kupata kura 95 kati ya kura halali 125 zilizopigwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF akitangaza majina ya washindi wa uchaguzi huo.

 

Richard Wambura akiwa na Wallace Karia baada ya matokeo kutangazwa

 

Wallace Karia akiapa Kiapo cha Utii kuwa Rais wa TFF.

 

Richard Wambura akiapa kuwa Makamu wa rais wa TFF.

Matokeo ya Urais

Kura ziliopigwa-128

Zilizoharibika-3

Iman Madega- 8

Mwakalebela- 3

Emmanuel Kimbe- 1

Shija Richard- 9

Ally Mayay- 9

Wallace Karia- 95 (Mshindi)

PICHA NA MUSA MATEJA  | GPL| DODOMA

VIDEO YA MATOKEO HAYO


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment