The House of Favourite Newspapers

Wananchi Gongo la Mboto Kutembezewa Kipigo na Askari, DC Mjema Afunguka

0

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema Jumanne hii ametembelea maeneo ya Ukonga jijini Dar es salaam baada ya siku ya jana taarifa kuzagaa katika mitandao ya kijamii kwamba maeneo hayo sio shwari kwani askari wa kutuliza ghasia (FFU) walikuwa wanawapiga wananchi wa maeneo hayo kwa madai walishiriki kumuuwa askari mwenzao.

DC baada ya kufika maeneo hayo, amewaamuru Askari wa kutuliza Ghasia (FFU) waondoke kwenye maeneo ya wananchi katika eneo lote la Ukonga kuanzia sasa na wasiwabughudhi wananchi.

Mjema amesema hayo leo Jumanne baada ya kutembelea eneo la Ukonga Mombasa lililokumbwa na vurugu kwa siku mbili baada ya kudaiwa kuuawa kwa askari wa FFU jambo lililofanya askari kupiga watu hovyo na kuzua hofu.

Amesema wananchi waliojeruhiwa na askari hao wajiorodheshe majina yao na askari waliohusika kuwapiga raia wachukuliwe hatua za kinidhamu kwani hawakupaswa kujichukulia sheria mkononi kama wananchi waliohusika kumuua askari mwenzao.

Katika eneo hilo hali si salama kwa kuwa maduka na huduma za kijamii zimesimama wananchi wako barabara wakiandamana.

Mmoja wa wananchi wa eneo hilo, Issa Salehe amesema jana Jumatatu usiku askari wa FFU walivamia eneo lake la biashara wakachukua wakala kisha wakavunja vyombo vyote.

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android Bofya ===> Google Play

iOS Bofya ===>Apple Store

Leave A Reply