The House of Favourite Newspapers

Shabani Ngao Aibuka Mshindi wa Pikipiki Droo ya Nne ya Shinda Nyumba

0
Wanenguaji wa Kundi la Black Warriors wakitoa burudani wakati wa droo hiyo.

 

Wasomaji wa Magazeti ya Global Publishers wakitumbukiza kuponi za shinda nyumba kwenye ndoo malum ya kukusanyia kuponi hizo.

 

Kuponi za Shinda Nyumba zikichanganywa.

 

 

Kuponi zikiendelea kuchanganywa.

 

MC Chaku akisoma jina la Mshindi wa pikipiki kwenye droo ya nne ya Shinda Nyumba, Shabani Ngao wa Tabata Dar.

 

 

Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, bakari Majjid (kushoto) akijadili jambo na Mhariri wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli.

 

Mwakilishi kutoka TING, James Rugaimukama akizungumza na mteja.

 

Elvan Stambuli akiwahamasisha wananchi kushiriki Shinda Nyumba wakati akizungumza na vyombo vya habari baada ya kumalizika kwa droo hiyo.

 

Mr. Shinda Nyumba (kulia) na MC Chaku wakiwa na baadhi ya wadau waliojitokeza kwenye droo hiyo.

 

ILE droo ndogo ya nne ya shindani la bahati nasibu la Shinda Nyumba linaloendeshwa na Kampuni ya Global Publishers kupitia magazeti ya Championi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi, Risasi Mchanganyiko, Amani na Uwazi imefanyika katika Viwanja vya Mwinjuma vilivyopo Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Katika droo hiyo, Shabani Ngao (38) mkazi wa Tabata, Dar, ameibuka mshindi wa pikipiki mpya ambapo baada ya kupigiwa simu na MC Chaku aliyekuwa akiendesha droo hiyo, Shabani Ngao hakuamini mara moja kama kweli ameshinda pikipiki.

“Aaaaaa, aisee! sina hata la kusema, labda niwashauri wasomaji wasome magazet ya Global Publishers ili waweze kushinda kama nilivyoshinda mimi. Wasikate tamaa maana hata mimi sikujua kama nitashinda siku moja,” alisema Shabani kwa njia ya simu.

Katika shindano hilo ambalo linadhaminiwa na King’amuzi cha Ting, British Schools pamoja na Kampuni ya Simu za mkononi ya Tecno, washindi wengine waliopatikana.

Washindi wa ving’amuzi ni; Ringo Mboya mkazi wa Uyole Mbeya, Verus Kuyamba mkazi wa KCMC, Moshi, Roda Kimenyi mkazi wa Morogoro, Dkt. Ohemba wa Nchuka, Dodoma na Ally Ramnadhani Kazi wa Mburahati Dar es Salaam.

Mshindi wa Dinner Set ni; Peter C katua (41) mkazi wa Ialal jijini Dar es Salaam.

Mshindi wa SamrtPhone ni; Ally Khalifa Kachenje (55) mkazi wa Arusha.

PICHA NA RICHARD BUKOS | GLOBAL TV ONLINE

Leave A Reply