The House of Favourite Newspapers

Watoto wa Shule ya Lucky Vincent Wawasili KIA

0

WATOTO watatu wa Shule ya Msingi Lucky Vincent waliokuwa majeruhi wa ajali iliyotokea Karatu na kwenda kutibiwa nchini Marekani, tayari wamewasili asubuhi hii katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mjini Moshi.

Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent wakijiandaa kuwapokea watoto hao.

 VIDEO LIVE: Mapokezi ya Watoto wa Shule ya Lucky Vincent KIA


Watoto hao ambao ni Doreen, Sadia na Wilson waliokuwa wakitibiwa katika Hospitali ya Mercy, Sioux City, Marekani tayari wamewasili wa ndege ya Samaritan,s Purse wakitokea nchini humo baada ya kupata nafuu.

 

Wanafunzi wa Lucky Vincent wakijiandaa kuwapokea watoto hao.

 

Mamia ya wakazi wa Arusha, ndugu, jamaa, marafiki na viongozi mbalimbali wa serikali wamefika kwa ajili ya kuwapokea watoto hao. Baadhi ya viongozi hao ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, Mbunge Lazaro  Nyarandu makatibu tarafa wa mikoa na viongozi wa wilaya za mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

Ndege ilioyowabeba watoto hao ikitua KIA.

Watoto hao ni miongoni mwa wanafunzi wa shule ya Lucky Vincent walionusurika kifo katika ajali ya gari iliyotokea mkoani Arusha mwezi Mei mwaka huu, ambapo inakadiriwa idadi ya waliopoteza maisha ni 33 ikijumuisha wanafunzi na walimu waliokuwa katika gari hilo.

Mtandao wa Global Publishers unawashukuru madaktari na kila aliyetenga muda wake kuwaombea na kuchangia chochote kusaidia matibabu ya watoto hao.

Shamrashamra Mapokezi ya Watoto wa Shule ya Lucky Vincent KIA

Leave A Reply