The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Wazee Simba Wakinukisha Sakata la Mo Kujiondoa & Udhamini wa SportPesa

0

 

Sakata la mabadiliko ya katiba ya Klabu ya Simba ambayo yanatajwa kuwa yanaweza kuifanya klabu hiyo kuingia katika uwekezaji wa kununuliwa kwa hisa sasa yamefikia kwenye ‘moto’ mkali.

Baraza la Wazee la Simba, limeibuka na kusema mabadiliko ya katiba ya klabu hiyo yanafanyika kihuni. Simba ilikuwa katika mchakato wa kubadili baadhi ya vipengele vya katiba ili iweze kuuza hisa zake na tayari mfanyabiashara na mwanachama wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’ alishajitokeza kununua hisa asilimia 51 akiwekeza shilingi bilioni 20.

Wazee hao wametaka mchakato kwa hatua sahihi ufuatwe badala ya uharakishaji wa mambo kama ambavyo inataka kufanyika sasa na wamemuandikia barua Rais John Pombe Magufuli.

Mratibu wa Baraza la Wazee la Simba, Felix Mapua amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwamba wameamua kumuandikia barua Rais Magufuli, wakiomba kumuona.

“Tunaona mambo yanapelekwa haraka na kihuni, tumeamua kumuandikia barua Rais Magufuli kupitia kwa Waziri wa michezo, Dk Mwakyembe.

“Tunaomba kumuona Rais Magufuli, tunaona hata iwe kwa dharura. Hata kidogo hatukubaliani na mambo yanavyokwenda na hatufurahi hata kidogo.

“Simba ni kubwa sana, kubwa kuliko hata Mohamed Dewji. Hivyo hatuwezi kukubali mambo yaende namna hii,” alisema na kuongeza:

“Kuna wahuni wachache wanataka kupeleka mambo kibabaishaji, tunampa rais wetu Aveva kuwa aendelee na mwendo huu huu alionao, hapa kuna tatizo na ndiyo maana tayari tumesharipoti Takukuru juu ya hiki kinachoendelea.”

Baada ya hapo mwanachama mwingine wa klabu hiyo, aliyejitambulisha kwa jina la Bosi Matola mwenye kadi namba 080 alisema: “Kilichonileta hapa ni kumpongeza rais wangu Aveva kwa kuingia mkataba na kampuni hiyo ya mapesa, kijana wetu Mo amelipa mishahara kwa miezi nane tu anaidai klabu shilingi bilioni 1.4, sasa angekaa miaka mitano si angechukua jengo.”

FUATILIA TUKIO ZIMA HAPA

Leave A Reply