The House of Favourite Newspapers

JPM Kuongoza Mkutano wa Kimataifa na Kihitosria – Video

RAIS  John Magufuli anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuia ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kuanzia Agosti 17 mwaka huu hadi Agosti 17, 2020 ambapo zaidi ya watu 1,000 wanatarajiwa kushiriki mkutano huo unaotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam.

 

Taarifa hiyo imetolewa leo, Jumatano na Waziri wa Mambo ya Nje, Profesa Palamagamba Kabudi alipokutana na watendaji wakuu wa vyombo vya habari na kusema Rais Magufuli anachukua nafasi hiyo kutoka kwa mtangulizi wake, Rais wa Namibia Hage Geingob ambaye amemaliza muda wake.

 

Mkutano huo wa 39 unatarajiwa kufanyika Agosti 17 na 18 na kuhudhuriwa na wakuu wa nchi 16 wanachama wa jumuiya hiyo na utatanguliwa na vikao vya mawaziri na makatibu wakuu wa nchi wanachama wa SADC na maonyesho ya viwanda yatakayofanyika katika ukumbi wa Mlimani City.

 

Mkutano mkuu wa SADC utafanyika jijini Dar es Salaam ikiwa ni miaka 16 tangu ufanyike mwingine kama huo. Mara ya mwisho kwa Tanzania kuandaa mkutano wa SADC ilikuwa mwaka 2003 wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

 

Kabudi amesema mwandishi wa habari Emmanuel Buhohela ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Habari, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

MSIKIE KABUDI

Comments are closed.