The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Aongoza Mazishi Kitaifa Ukara – Video

WAZIRI Mkuu,  Majaliwa Kassim Majaliwa,  ameongoza mazishi ya miili tisa iliyozikwa katika makaburi ya pamoja katika viwanja ya Shule ya Sekondari ya Bwisya ambapo miili minne kati yake haikutambuliwa,  na mitano ndugu waliridhia izikwe na serikali.

Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akiweka shada la maua.

Akizungumza na wananchi waliofika katika viwanja vya Bwisya amesema kuwa kivuko kilizidisha abiria ambapo kilibeba watu zaidi ya 260 na mizigo iliyozidi huku uwezo wake ni tani 25 pekee ambazo ni sawa na abiria 101 na magari matatu.

“Mimi nitaendelea kubaki Ukara ili kusimamia mazishi ya miili ya wataokuwa wanapatikana hadi hapo tutakapohitimisha zoezi la uokoaji ikiwa tumefanikiwa kuokoa watu wotem” amesema.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema miili ambayo imeopolewa hadi leo mchana ni ya watu 224,  wanawake wakiwa 125 na wanaume 71 watoto wa kike 18 watoto wa kiume 10, na miili saba ilikuwa bado haijatambuliwa.


Ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama Alhamisi mchana Septemba 20, 2018 imechukua maishaya watu 224 hadi sasa huku uokoaji ukiendelea ambapo Rais John Magufuli ametangaza maombolezo ya siku nne na bendera za taifa kupepea nusu mlingoti.

Comments are closed.