The House of Favourite Newspapers

Hotuba ya Waziri Mkuu Bungeni Dodoma Leo – Video

0

Waziri Mkuu ameliomba Bunge liidhinishe TZS bilioni 116.8 kwa ajili ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake kwa matumizi ya mwaka 2021/2022. Kati ya fedha hizo TZS bilioni 93.3 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na TZS bilioni 23.5 ni kwa ajili ya maendeleo.

 

 

“Katika mwaka 2021/22 serikali itaimarisha usimamizi na utekelezaji wa mipango na miradi ya maendeleo, matumizi ya fedha za umma na uwajibikaji, itatumia rasilimali zilizopo katika shughuli za uzalishaji mali kuchochea ukuaji wa uchumi.

 

 

“Wastani wa idadi ya watu wanaopata maji kwa mijini ni asilimia 86 na asilimia 73. 3 kwa vijijini, hadi Machi 2021 sh. Bilioni 1.3 zimetumika na kazi ya usambazaji maji vijijini inaendelea kwa kasi.

 

 

“Hadi kufikia JanuarI 2021, Sh. Bilioni 178 zimetumika kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu muhimu katika shule za msingi, sekondari na vyuo vya maendeleo ya wananchi, uimarishaji wa miundombinu ya elimu utasaidia kuongeza ubora wa elimu inayotolewa.

 

 

“Utekelezaji wa mpango na bajeti ya serikali mwaka 2020/21 umekuwa wa mafanikio makubwa sana ikiwemo kugharamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati, moja ya miradi hiyo ni ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa.

 

 

“Natoa rai kwa Watanzania wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kulinda na kuendeleza mafanikio tuliyoyapata. “Nitoe rai kwamba sekta binafsi ilete mpango mahsusi kuhusu namna ambavyo itaunga mkono mipango na mikakati ya Serikali ikiwa ni pamoja na kutengeneza ajira milioni nane katika kipindi cha miaka mitano.

 

 

Tanzania imefanikiwa kudhibiti wadudu waharibifu wa mazao wajulikanao kama Nzige ambao wamekuwa ni tishio kwa mazao mbalimbali ya chakula katika ukanda wa Afrika Mashariki.

 

 

“Nitumie nafasi hii kulipongeza shirika la ndege Tanzania (ATCL) kwa kuanzisha safari za kwenda nje ya nchi, Guangzhou China, Safari hizo zitakuwa chachu ya kuimarisha biashara, utalii na Ajira.

 

 

“Sambamba na uimarishaji wa miundombinu ya usafiri wa anga Serikali imekamilisha malipo ya ununuzi wa ndege mpya tatu, ndege hizo zinatarajiwa kuwasili mwaka 2020/22 na hivyo kuwezesha Serikali kuwa na ndege zake 12.

 

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema hali ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI nchini imepungua kutoka watu 130,000 kwa mwaka 2001 hadi 77000 kwa mwaka 2019.

 

 

Leave A Reply