The House of Favourite Newspapers

LIVE: Waziri Mkuu Azindua Kampeni ya Kuichangia Serengeti Boys

0

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amezindua rasmi Kampeni Maalum ya kuichangia Timu ya Taifa ya Vijana Chini ya Umri wa Miaka 20, Serengeti Boys ili kufanikisha kuisaidia timu hiyo ifanye vizuri kwenye mashindano ya Kimataifa hadi kufikia Michuano ya Kombe la Dunia.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo ambayo imefanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena ya jijini DFar es Salaam usiku huu, Majaliwa amewataka wadau wote wa michezo nchini kuisaidia timu hiyo kwa hali na mali ili iweze kufikia malengo yake ambayo ni mafanikio kwa Taifa katika nyanja ya soka.

Pia Majaliwa amewataka Sertengeti Boys wajitume kufanya mazoezi kwa bidii ili kujiweka sawa katika michezo inayowakabili sambamba na kuliwakilisha vyema taifa.

“Niwasihi Watanzania wajitoe kuisaidia Serengeti Boys ambayo kwa sasa inapeperusha Bendera ya Tanzania nje ya Mipaka ya nchi.

“Niwasihi wanamichezo wenzangu, tuna matumaini makubwa na Serengeti Boys, naamini mtatuunga mkono ili tuisaidie vyema timu hii ipeperushe vyema bendera yetu, naamini Serengeti Boys watashinda michezo yote ambayo imepangwa kwenye kundi letu pamoja na michuano ya Afcon itakayofanyika huko Gabon mwezi Mei.” Amesema Kassim Majaliwa.

Leave A Reply