LIVE: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Afika Mnazi Mmoja Kusikiliza Kero za Wafanyabiashara wa Kariakoo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amefika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wake na wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo leo Mei 17, 2023 kusikiliza kero zao baada ya wafanyabiashara hao kugoma kufungua maduka yao kwa muda wa siku tatu mfululizo, kutokana na malalamiko mbalimbali ikiwemo kudai kunyanyaswa na maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Akiwa viwanjani hapo, Majaliwa amewataka wafanyabiashara hao kuzungumza kero zao zote zilizosababisha wakafikia hatua hiyo, na kuwahakikishia kwamba hakuna atakayedhurika kwa kuzungumza ukweli, huku akisisitiza kwamba serikali haifurahishwi kuona wafanyabiashara hao wanafanya kazi zao kwa manung’uniko.