The House of Favourite Newspapers

FT: Yanga 2-0 Aigle Noir Uwanja Wa Mkapa

0

MECHI ya kirafiki imemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Aigle Noir ya Burundi Uwanja wa Taifa kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, bao limefungwa na Tuisila Kisinda dakika ya 38.
Bao la pili la pili limefungwa kupitia kwa Michael Sarpong dakika ya 59

HT: Yanga 1-0 Aigle
Zinaongezwa dakika 3
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zinakamilika
Dakika ya 44 Aigle wanapeleka mashambulizi Yanga
Dakika ya 38 Gooooal, Tuisila Kisinda kwa pasi ya Fei Toto
Dakika ya 38 Kaseke anakosa bao la wazi
Dakika ya 36 mlinda mlango wa Aigle, Erick anapewa huduma ya kwanza
Dakika ya 30, nyota wa Aigle, Koffi anaonyeshwa kadi ya pili ya njano na kufanya aonyeshwe kadi nyekudu,
Dakika ya 23 Kibwana Shomari anamwaga maji yanakutana na mikono ya kipa wa Aigle

Dakika ya 20,Tuisila ndani ya 18 anampa Yassin Mustapha ambaye anamwaga maji yanakutana na kichwa cha Sarpong hakizai matunda

Dakika ya 13 Aigle wanaanzisha mashambulizi kwenda Yanga

Dakika ya 10 Koffi Kouassi wa Aigle alionyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea rafu Kisinda

Dakika ya 3 Michael Sarpong alisababisha kona ambayo haikuzaa matunda

UWANJA wa Mkapa

Mchezo wa kirafiki wa kimataifa

Yanga 0-0 Aigle Noir

Leave A Reply