The House of Favourite Newspapers

Manara Awaomba Radhi Yanga ‘Niliteleza’ – Video

0

MSEMAJI wa Yanga, Haji Manara leo Jumanne, tarehe 7 Septemba 2021 amewaomba radhi wanachama na mashabiki wa timu hiyo kwani “kuna mahali niliteleza.”

 

Manara amewaomba radhi , alipokaribishwa rasmi makao makuu ya Yanga, Jangwani jijini Dar es Salaam baada ya kujiunga nao hivi karibuni akitokea kwa watani zao Simba.

 

Amepolekewa na wazee wa timu hiyo ambapo kabla ya kuingia ndani ya ofisi hizo zilizopo mtaa wa Jangwani na Twiga, Manara alinawishwa maji ikiwa ni ishara ya kusafishwa kutoka huko alikokuwa kuingia Yanga.

 

“Nimerudi kwenye klabu iliyonilea na ya maisha yangu. Wazazi wangu licha ya kucheza na kufanya kazi hapa lakini ndiyo ilinilea.”

 

“Wazee wangu kama kuna mahali lazima niliteleza kiungwana kabisa naombeni msahama wa dhati kabisa. Lazima niliteleza tu na mchukulie kuteleza kwangu ndiyo ilikuwa fursa ya kuja kufanya kazi kwa mabingwa wa kihistoria ‘home of championi,” amesema Manara

 

Manara amejiunga na Yanga akitokea kwa watani zao Simba nayo ya jijini humo alikoitumikia kama shabiki na msemaji kwa kipindi kirefu na kwa mafanikio makubwa.

 

Alianza kuzungumza kwa kuwashukuru mashabiki, wanachama na viongozi wa timu hiyo jinsi walivyompokea katika maeneo mbalimbali ikiwemo mitandaoni.

 

“Katika siku ngumu ni leo, unapokelewa na watu ambao wewe unapaswa wakupokea, kwa mila na desturi wazee wanapokewa na vijana ila leo nimepokelewa na wazee wangu.”

 

“Deni hili pia ninalo kwa wanachama na mashabiki wa Yanga nchi nzima, kwa jinsi nilivyofanya kazi kule na kwa mapokezi siku ya kilele cha wiki ya mwananchi na mitandaoni, nina deni kubwa na halina budi kulipwa kwa kufanya kazi kwa kujitoa sana, kufanya kazi weledi mkubwa,” amesema

 

“Katika siku ngumu ni leo, unapokewa na watu ambao wewe unapaswa wakupokee, kwa mila na desturi wazee wanapokewa na vijana ila leo nimepokelewa na wazee wangu.”

 

Manara amesema “deni hili pia ninalo kwa wanachama na mashabiki wa Yanga nchi nzima, kwa jinsi nilivyofanya kazi kule, kwa mapokezi siku ya kilele ya wiki ya mwananchi na mitandaoni, nina deni kubwa na halina budi kulipwa kwa kufanya kazi kwa kujitoa sana, kufanya kazi wa weledi.”

 

Msemaji huyo mwenye maneno mengi amesema, Yanga ni nyumbani kwani amezaliwa maeneo hayo ikiwemo kucheza ndani ta jengo hilo, kwenye vyumba vya wachezaji kwa maana hiyo “nimerudi kwelikweli nyumbani sehemu iliyonikuza.”

 

Awali, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha amemkaribisha Manara Yanga akisema Imani yake watafanya kazi pamoja kwa mafanikio makubwa “karibu sana nyumbani.”

 

Senzo na Manara waliwahi kufanya kazi pamoja wakiwa Simba na kila mmoja akiwa kwenye nafasi hizo hizo ambazo sasa wanazitumikia wakiwa Yanga.

 

Leave A Reply