Liverpool Yachapwa na Man United, Yatupwa Nje Fa Cup

HALI imekuwa mbaya zaidi kwa Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp baada ya jana usiku kutupwa nje ya michuano ya FA Cup kwa kichapo cha magoli 3-2 kutoka kwa Manchester United, mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Old Trafford, Uingereza.

 

Hii si habari njema kwa Liverpool kutokana na kuwa na mwenendo usioridhisha wakiwa wanaendelea kupokea vichapo.

 

Mohamed Salah alifunga bao la mapema dakika ya 18, goli ambalo halikudumu muda mrefu baada ya kinda Mason Greenwood kuisawazishia United dakika ya 26.

Kipindi cha pili Man United walicharuka na kufunga bao kupitia kwa Marcus Rashford dakika ya 48 na mfalme wa Misri, Salah akafanikiwa  kusawazisha dakika ya 58.

 

Kuingia kwa fundi Bruno Fernandes kuliipa faida United baada ya kufunga goli murua  kwa mkwaju wa faulo goli ambalo lilizima ndoto za Majogoo wa Jiji Liverpool, kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

 

Baada ya mchezo huo kocha wa Liverpool Klopp, amesema bado haelewi kwa nini walipoteza mchezo huo na kukiri wanahitaji kufanya kazi ya ziada ili kurudi kwenye ubora wao ambao watu wameuzoea.

 

Kwa matokeo hayo ya ushindi Manchester United wametinga raundi ya tano na watakutana na West Ham.

Kwa habari kama hizi, Pakua App ya Global kwenye Google Playstore, App Store.
⚫ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
⚫ ANDROID: http://bit.ly/38Lluc8
⚫ iOS: https://apple.co/3msGaf8


Toa comment