The House of Favourite Newspapers

Lojay Aachia ‘Moto’ Ikiwa ni Maandalizi ya Kuachia EP Mpya, ‘Gangster Romantic’

0

 

STAA wa Amapiano aliyetesa vilivyo na kibao chake ‘Monalisa’, Lojay sasa ameachia mtaani singo yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘MOTO’, ikiwa ni mwanzo wa kuelekea kutoa EP yake mpya GANGSTER ROMANTIC.

‘MOTO’ ni wimbo wenye kisa cha kimapenzi, ambao unanogeshwa na uzuri wa ala za muziki zinazorindima kwa kasi na taratibu zikipishana na kuleta ladha ya aina yake.

Prodyuza wa wimbo huo ni Lojay mwenyewe, huku umaliziwaji ukifanywa na Elementz na  AOD.

Mwongozaji wa video yake hiyo ni galacha, Des Gray kutoka Atlanta ambaye amepata kutia mikono katika kazi za mastaa wakubwa kama Quavo, Davido na Lil Baby.

Simulizi ya wimbo huo, ulioigizwa na Lojay mwenyewe, inaelezea kisa cha mapenzi, namna uhusiano ulivyoanza na kila aina ya nakshi kabla ya kuvunjika; imehaririwa kwa rangi ya samawati ili kuakisi uzito wa wimbo na kisa kilichopo ndani ya wimbo huo.

EP ijayo ya Lojay inawakilisha ulimwengu wenye misukosuko wa Lojay, unaoangaziwa na mambo ya shauku, tafakari ya kina, hofu kuu na mapenzi.

Ni tafakari ya kina juu ya mwaka uliopita wa maisha yake, huku Lojay akiwasilisha upya majarida yake ya dhati na maingizo ya hisia kuhusu mapenzi, maisha na huzuni katika shajara ya kusisimua, yenye tafakari, matarajio na fikira juu ya uhuru.

Wimbo wake wa ‘Canada’ alioutoa mwaka jana, akiwa amepiga kolabo na Kabza De Small na DJ Maphorisa, ulipata uungwaji mkono kutoka kwa Rolling Stone na DJ Target katika BBC Radio 1Xtra, huku ‘Leader’ alipongezwa na Jack Saunders wa BBC Radio 1.

Msanii huyo ataanza ziara nchini Australia mapema mwezi huu, ikiwa ni mwendelezo wa kung’arisha jina lake ulimwenguni akiwa ni staa anayetesa vilivyo kwenye mahadhi ya AfroBeats.

Stori: Joseph Shaluwa

 

Leave A Reply