The House of Favourite Newspapers

Lokosa Apata Dili Norway

0

IMEELEZWA kuwa, nyota mpya wa Simba, Junior Lokosa, yupo kwenye hesabu za kusajiliwa na timu ya Stromsgodset Toppfotball inayoshiriki Ligi Kuu ya Norway.

 

Raia huyo wa Nigeria akiwa amesaini dili la miezi sita ndani ya Simba akiwa ameletwa kwa ajili ya kuongeza nguvu katika michuano ya kimataifa, bado hajapata nafasi ya kucheza chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes.

 

Habari zinaeleza kuwa, timu hiyo ya nchini Norway ipo tayari kumnunua jumlajumla nyota huyo kwa dola 200,000 (sawa na Sh 461,633,000 za Kitanzania).

 

Spoti Xtra lilimtafuta Katibu Mkuu wa Simba, Arnold Kashembe kuzungumzia dili hilo, alisema kwa kifupi: “Ni mapema sana kuzungumza kwa sababu bado sijapata taarifa zozote juu ya jambo hilo.”

Stori na SAID ALLY,Dar

Leave A Reply