The House of Favourite Newspapers

Lord Eyez, Huna wa Kumlaumu!

0

NA OJUKU ABRAHAM | RISASI JUMAMOSI | MZEE BUNDUKI

SIKU zote maisha ni vile unavyotaka yawe na kila mmoja ana malengo yake. Lakini pia wapo wasio na malengo, wanaishi wakiwa hawajui nini kitatokea kesho na wala hawajisumbui kufikiria hivyo.

Hata hivyo, wapo walio na malengo, lakini wanashindwa kutimiza kwa sababu mbalimbali, kama vikwazo na changamoto wanazokutana nazo katika maisha, maana ili kufi kia mafanikio kunahitaji mapambano kwelikweli.

Maisha yana tabia ya kuwatenganisha ndugu, marafi ki na hata washirika. Unayesoma naye chekechea, shule ya msingi, sekondari na hata chuo kikuu, siye utakayekutana naye kazini na kwenye harakati zingine za maisha.

Watu waliosoma shule moja ya msingi, ukubwani hujikuta wakkituo itengana, wengine wakiendelea  ekondari, wengine wakibakia nyumbani, wengine wakiamua kujiingiza kwenye kilimo na mambo mengine ya maisha. Uzoefu unaonyesha wale wanaofanikiwa, kwa maana ya kujimudu katika maisha, huendelea kuwasiliana.

Ukisikia watu wanasema huyu jamaa nimetoka naye mbali, ujue wako katika mwelekeo mmoja, kwa maana kwamba hata kama wana tofauti kubwa ya kipato, lakini kipo kitu kinachowaleta pamoja. Katika harakati za kufatuta, inafi kia kipindi baadhi ya watu huwakimbia watu wanaowafahamu.

Na wengine huwaona wenzao waliokua au kusoma pamoja kama wanaojidai, pale wanapowaona wamefanikiwa. Hili ni kosa la asili ambalo binadamu tunalo, tunadhani kwa kuwa huyu tulisoma naye, au tulikuwa kazini pamoja, basi mafanikio yake tule wote na inapokuwa tofauti, tunakuwa na maneno mengi yenye kuonyesha mtu huyo ana dosari.

Nimeanza hivi nikirejea maneno ya memba wa zamani wa Weusi, Lord Eyez ambaye katika mahojiano na kituo kimoja cha redio, alionekana wazi kuwa na kinyongo na wenzake, ambao bahati nzuri hivi sasa mambo yao yamekaa levo!

Hawa ni vijana waliokaa pamoja, wametoka wote Arusha, lakini muziki umewafanya wajulikane kama memba wa kundi moja, ingawa mara kwa mara wote wamekuwa wakisema kuwa Weusi siyo kundi, isipokuwa ni kampuni ambayo inaonekana kushikiliwa na ndugu wawili, Joh Makini na Nikki wa Pili!

Wote tunajua kuwa Lord Eyez ana uwezo mkubwa katika kufanya muziki, lakini siyo viziwi, kwani tumesikia mara nyingi kuwa alijiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya.

Tabia hii ilimpotezea vitu vingi, ikiwemo umakini wake katika kazi, kiasi kwamba wenzake wakaona ni vyema akakaa pembeni kidogo, maana Weusi tayari walikuwa ni brand mbele ya jamii. Kuwepo kwa mtu mwenye tabia isiyofaa siyo kitu ambacho kampuni yoyote inayotaka kukua ingehitaji, kwa hiyo halikuwa kosa lao kumweka pembeni, bali matakwa ya kukua ndivyo yanavyotaka.

Lord Eyez kusema kuwa Weusi wana ubinafsi na mambo mengine kama alivyosema, ni kama kutaka kumtwisha mzigo wa maisha yako mtu mwingine asiyehusika.

Kama kushindwa kusonga mbele katika maisha kumemshinda, ni kosa lake mwenyewe na anayestahili lawama ni yeye.

Tabia ya watu kuwalaumu wenzao baada ya kukwama katika maisha yao imekuwa ikiongezeka, maana mtu anaona kwa sababu tu tulifanya kazi wote, tulisoma pamoja, tulikuwa kundi moja, tumetoka kijiji kimoja, basi eti mwenzio abebe msalaba wako.

Sikatai, kuomba msaada kwa mtu unayemfahamu ni kitu cha kawaida, lakini siyo kumpa lawama anaposhindwa kukidhi matakwa yako, hasa kama ulifanya ujinga katika kujenga maisha yako, kama ilivyo kwa Lord Eyez.

Ningemshauri huyu msanii kuyaangalia upya maisha yake maana muda wa kujirekebisha bado upo. Aache kuwalaumu watu kwa makosa yake. Ray C, Chid Benz ni mifano tosha kwake!

Keep It Up Weusi!

Leave A Reply