The House of Favourite Newspapers

Lori Lateketea Tunduma

0

Lori la mizigo aina ya Scania lenye namba za usajili T 887 CWN lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Tunduma mkoani Songwe, limeteketea kwa moto pembezoni mwa mizani ya Mpemba nje kidogo ya Mji wa Tunduma.

Gari hilo lililokuwa na mizigo mchanganyiko ya madukani limeteketea asubuhi hii ya leo, Jumatano, Julai 28, 2021 huku chanzo cha moto huo bado kikiwa bado hakijajulikana. Kikosi cha Zimamoto na uokoaji wanaendelea kuudhibiti moto huo.

Aidha, chanzo cha moto huo bado hakijajulikana huku madhara yaliyotokana na moto huo ni kuteketa kwa gari na mizigo iliyokuwemo katika gari hilo. Hakuna mtu aliyeripotiwa kufariki wala wala kujeruhiwa.

Taarifa Zaidi zinakujIia.

Leave A Reply