The House of Favourite Newspapers

Lowassa Afuata Dhamana ya Mbowe, Wenzake Mahakamani – Video

Lowassa alipowasili mahakamani hapo.

MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na viongozi wenzake watano wa chama hicho leo wanatarajiwa kurejeshwa tena katika Mahakama ya Kisutu, Dar leo Machi 29, 2018 asubuhi ili kuendelea na kesi inayowakabili.

 

Mbowe na wenzake watafikishwa mahakamani hapo wakitokea mahabusu ya Segerea ambapo wanakabiliwa na mashtaka manane yakiwemo kufanya maandamano yaliyosababisha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha NIT, Akwilina Akwiline, Februari 16, mwaka huu, uasi na kuhamasisha chuki.

Baada ya viongozi hao kufikishwa mahakamani hapo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa na viongozi wengine wa chama hicho walifika mahakamni hapo ili kusikiliza kesi hiyo na kufanya jitihada za kuomba dhamana kwa watuhumiwa hao leo.

Kesi ya Mbowe, Chadema: Lowassa Atinga Mahakamani, Ulinzi Mkali!

Edward Lowassa, Prof. Abdallah Safari na Fredrick Sumaye wakiwa mahakamani hapo.

Viongozi wengine waandamizi wa chama hicho wanaoshtakiwa katika kesi hiyo ni: Katibu Mkuu Dkt. Vincent Mashinji, John Mnyika, Salum Mwalimu, Mch. Peter Msigwa na Ester Matiko ambapo wote wamefikia kwenye chemba ya mahakama ambapo kesi hiyo itasikilizwa.

Updates:

Mpaka sasa Mbowe na wenzake hawajafikishwa katika eneo la Mahakama, tetesi zinadai kuwa ‘magereza hawana gari la kuwaleta mahakamani.”

VIDEO: WASIKIE HAPA CHADEMA WAKIFUNGUKA

Comments are closed.