The House of Favourite Newspapers

Edward Lowassa Afunguka Alivyohojiwa na DCI, Aachiwa kwa Dhamana (VIDEO + PICHAZ)

0
Polisi wakiimarisha ulinzinje ya lango la Makao Makuu ya Polisi wakati Lowassa alipokuwa akihojiwa.

 

DAR ES SALAAM: Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa amefunguka kuhusu alivyohojiwa kwa saa nne katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi  wa Makosa ya Jinai (DCI) ambapo baada ya kuhojiwa ameachiwa kwa dhamana na kuondoka makao makuu ya polisi majira ya saa 8.

 

Akizungumza nyumbani kwake, Oyster Bay jijini Dar mara baada ya kutoka Makao Makuu ya Polisi, Lowassa amesema aliitwa kuhusu kauli aliyoitoa ya viongozi wa dini ya Kiislam wa Zanzibar (Uamsho) kuendelea kusota rumande kwa miaka kadhaa sasa kauli ambayo inadaiwa kuwa kuwa ni ya uchochezi.

 

Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Mashinji, Edward Lowassa na mkewe Regina Lowassa.

“Nimeitwa kuhojiwa kuhusu hotuba niliyoitoa hivi karibuni wakati wa futari kwa Mbunge Waitara. wengine wameielewa kama ni ya uchochezi.

“Nimejieleza wachakuchua maelezo yangu ambayo wanayatafakari hivyo tutakutana tena Alhamisi saa 6:00 mchana.

“Hivyo niwatake wanachama wa Chadema wasiwe na hofu, tupo imara.” alisema Lowassa

Wakati wa futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) Lowassa alisema aliwaahidi wananchi endapo angechaguliwa kuwa rais angewatoa mashehe hao siku hiyo hiyo lakini anashangaa viongozi hao wa dini wanavyoendelea kusota rumande mpaka sasa bila kufahamu kosa lao.

 

Lowassa akifunguka, wa kwanza kushoto ni Mwanasheria wa Chadema Peter kibatala

 

Akizungumzia suala hilo, Mwanasheria wa Chadema, Peter Kibatala amesema Lowassa amejidhamini mwenyewe na ametakiwa kuripoti tena Alhamisi saa 6.00 mchana.

Kibatala amesema Lowassa amehojiwa kwa kosa la uchochezi na ameandika maelezo ya onyo juu ya kauli aliyoitoa wakati wa futari iliyoandaliwa na mbunge huyo.

Wanahabari wakifuatikia tukio hilo.

 

“Mzee amehojiwa kwa kile wanachokiita kauli ya uchochezi aliyoitoa Juni 23, mwaka huu  wakati wa futari iliyoandaliwa na Waitara. Baada ya kuhojiwa ameandika maelezo ya onyo na atatakiwa kuripoti tena Alhamisi, Juni 29,” amesema Kibatala.

TAZAMA VIDEO LOWASSA AKIZUNGUMZA

Leave A Reply