Lowassa Aonesha Mahaba Yake kwa Simba Taifa

JUMAMOSI ya Februari 25, 2017 timu za Simba na Yanga zilikuwa zikiumana kwenye mpambano mkali wa kukata na shoka kati ya watani hao wa jadi ambapo Simba waliibuka kidedea kwa kuikung’uta Yanga mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam lakini kivutio kikubwa kilikuwa ni uwepo wa waziri mkuu mstaafu na mgombea urais kwenye uchaguzi wa 2015 kwa mwavuli wa Ukawa, Edward Lowassa.


Mashabiki wa Simba wakimshangilia Lowassa aliyekuwa akiwapungia mkono wakati wa mechi.
Lowassa akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe jukwaani wakati mechi ikiendelea.
Lowassa ambaye alikuwa amekaa kwenye jukwaa kuu, upande wa Simba alishindwa kuficha mahaba yake kwa klabu hiyo yenye maskani yake Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo ambapo mara kwa mara naye alikuwa akionesha kushangilia na zaidi alionekana kuwa na furaha zaidi baada ya mchezo kumalizika, Simba ikishinda kwa mabao mawili, yaliyofungwa na Laudit Mavugo na Shiza Kichuya.


Comments are closed.