The House of Favourite Newspapers

Lowassa Ashiriki Kuaga Mwili wa Mtoto wa Mwakasege

WAZIRI Mkuu wa zamani na Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa jana Jumanne, Oktoba 16, 2018 aliungana na ndugu, jamaa, marafiki na waombolezaji katika ibada ya kuaga mwili wa Joshua Mwakasege ambae ni mtoto wa Mchungaji, Mwalimu wa Christopher Mwakasege.

 

Ibada hiyo ilifanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam ambapo Lowassa aliongozana na mkewe, Mama Regina Lowassa.

 

Joshua alifariki dunia Oktoba 11, 2018 katika Hospitali ya Aga Khan baada ya kuugua ghafla wakati akiwa kazini. Mwili wa Joshua umesafirishwa kuelekea Tukuyu mkoani Mbeya kwa ajili maziko.

BREAKING: Basi lilivyotumbukia mlima kitonga leo!

Comments are closed.