The House of Favourite Newspapers

Lowassa, Gambo Uso kwa Uso Mazishi ya DC Molloimet – Picha

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo,  amekutana uso kwa uso na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu na mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015, Edward Lowassa, katika mazishi ya Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Luteni Mstaafu Lepilal Ole Molloimet.

Luteni Molloimet ambayea aliwahi pia kuwa Mbunge wa Monduli alifariki dunia Jumapili iliyopita na alizikwa jana wilayani Longido.

Mwishoni mwa mwaka jana, Gambo alidai amepata ujumbe kutoka kwa Edward Lowassa ambaye aliomba kukutana na Rais Magufuli ili amweleze adhima yake ya kurudi Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Chadema ambako alihamia wakati wa mchakato wa kuwania urais kwenye uchaguzi Mkuu wa 2015.

Kufuatia kauli hiyo, Lowassa alikana kuomba kukutana na Magufuli huku akidai kauli hizo za Gambo hazikuwa na mashiko.

Hata hivyo, mwanzoni mwa mwaka huu, Lowassa alikutana na Rais Magufuli, Ikulu, jijini Dar es Salaam huku tetesi zikisambaa kuwa alitaka kurejea hamia CCM lakini alikana madai hayo huku yeye na chama chake (Chadema) wakidai rais ndiye alikuwa akimshawishi kurudi CCM.

Comments are closed.