The House of Favourite Newspapers

Lowassa, Kinana, Polepole, Mbowe Kukutana Uso Kwa Uso Kesho

0

ALIYEKUWA mgombea wa urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Ngoyayi Lowassa; Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana; Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole na  Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe wanatarajiwa kukutana  katika kongamano litakalohusu Demokrasia na Siasa za Ushindani Nchini.

 

Mwenyikiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Ilala, Makongoro Mahanga, akizungumza na wanahabari.

Kongamano hilo litafanyika katika ukumbi wa Anartouglou ulioko Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam kuanzia saa mbili.

 

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyikiti wa Chadema Wilaya ya Ilala, Makongoro Mahanga,  amesema kuwa nia ya kongamano hilo ni kuwafahamisha wananchi na wadau wengine kuwa ushindani wa kisiasa ni jambo linalokubalika duniani kote na pia kujenga ufahamu kuhusu dhana ya ushindani wa kidemokrasia.

 

Mmoja wa waratibu wa kongamano hilo, Baraka Mwago, naye akifafanua jambo.

“Wapo wananchi wengi ambao bado hawajaelewa  vyema kwamba ushindani wa kisiasa siyo uadui na wala siyo kosa kisheria kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi,” alisema.

 

Aliongeza kuwa  kongamano hilo linatarajiwa kuwakutanisha viongozi wote wa vyama vya siasa ili  kuzungumza  juu ya umuhimu wa demokrasia katika vyama vya siasa.

 

“Kesho katika kongamano hili hatutazungumzia masuala ya vyama vyetu wala mitazamo yetu bali tutazungumzia demokrasia tu na hatutazungumza kitu chochote kuhusu vyama vyetu kwenye kongamano hilo,” alisema Makongoro.

 

Kutoka kushoto ni mmoja wa waratibu wa kongamano hilo, Allen Mazoko, Makongoro Mahanga na Baraka Mwago.

 

Alisisitiza kwamba waandaji wa kongamano hilo ni Chadema  kupitia Wilaya ya Ilala ambao ndiyo wamewapelekea barua za mialiko viongozi wote wa vyama vya siasa  nchini  na wadau wengine zikiwemo taasisi za haki za binadamu.

Miongoni mwa wazungumzaji wakuu wa kongamano hilo ni Deus Kibamba, Jenerali Ulimwengu, Zitto Kabwe, Harold Sungusia na wengine.

NA DENIS MTIMA/GPL  

Leave A Reply