The House of Favourite Newspapers

Lucky: Napenda sana kucheza na mbwa

0

KAMA kawaida, Mpaka Home inazidi kuchanja mbuga kutembelea mastaa mbalimbali Bongo. Wiki hii, paparazi wa Mpaka Home alisafiri hadi Mkoa wa Pwani-Kwa Mathias, nyumbani kwa mwigizaji Luckyness Mokiwa ‘Lucky’.

Kwa wale wanaotaka kumjua zaidi, ndiye aliyecheza filamu za; Bad Lucky, Second Wife, Rudi Kaburini, Identity Card alizoshirikishwa lakini alizozalisha mwenyewe ni No Stuck on You na Muhanga.

Mazungumzo yake na Mpaka Home nyumbani hapo yalikuwa hivi:

Mpaka Home: Kwanza wasomaji wa safu yetu ya Mpaka Home wangependa kujua hapa unaishi na nani?

Lucky: Nipo mimi, mume wangu, dada na kaka mmoja anayenisaidia kazi za nyumbani. Ila mume wangu mara nyingi anakuwa nje ya nyumbani kikazi.

Mpaka Home: Ukiamka asubuhi ratiba yako ikoje katika siku ambazo unakuwa huna mtoko?

Lucky: Nikiamka cha kwanza ni kufanya maombi kumshukuru Mungu kutuamsha salama. Baada ya hapo usafi wa mwili wangu kwanza kisha mazingira ya nyumbani halafu naandaa chai na mambo mengine yanafuata.Mpaka Home: Naona mbwa hapa, nani huwa anawahudumia? Unapenda sana mbwa?

Lucky: Ki ukweli nawapenda sana husasan mbwa wangu Queen. Nawahudumia ila zaidi mume wangu anawajali sana na kuwafanyia usafi kila wiki na chanjo. Mimi zaidi napenda sana kucheza nao.

Mpaka Home: Nguo za shemeji huwa unafua mwenyewe na kumpigia pasi au unamuachia dada akufanyie vyote?

Lucky: Hahaha hapana. Huwa nafua mwenyewe na kumpigia pasi. Mume wangu kwanza anapenda vitu hivyo nimfanyie. Tena si nguo tu, wakati mwingine huwa napenda kumsaidia dada kufanya usafi nyumbani maana na mimi mwenyewe mara nyingi nashinda nyumbani hususan kipindi hiki ambacho nalea.

Mpaka Home: Naona nje kuna mabanda ya kuku, kuku unafuga wa aina gani? Unao wangapi? Nani anawahudumia?

Lucky: Ninao kuku 135 wa kienyeji pia ninafuga na kanga, wapo kama 23 na njiwa15. Mara nyingi nawahudumia mwenyewe labda nikiwa  nimetoka, kuna kijana huwa ananisaidia.

Mpaka Home: Huyu mtoto mdogo anaitwa nani, una mwingine au ndiyo huyuhuyu?

Lucky: Anaitwa Tayana. Nina mwingine anaitwa Junior amemaliza kidato cha nne pale Sekondari ya Filbert Bayi .

Mpaka Home: Nikushukuru sana Lucky, tutaonana siku nyingine.

Lucky:  Asante karibu tena.

Leave A Reply